TARURA yaridhishwa na ujenzi Barabara ya Kidabaga-Bomang’ombe Kilolo

NA MWANDISHI WETU

WAJUMBE wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Mhandisi Florian Kabaka wamekagua Ujenzi wa Barabara ya Kidabaga - Boman g’ombe wilayani Kilolo, Iringa na kuridhishwa na ujenzi.
Akiwa wilayani Kilolo katika ziara ya Ukaguzi wa Mradi wa Barabara za “Agri-Connect “, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Florian Kabaka ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa Barabara ya Kidabaga -Bomang'ombe iliyojengwa kwa kiwango cha lamii yenye utefu wa kilomita 18.3

Mhandisi Kabaka amebainisha kuwa lengo la Serikali kupitia TARURA nikuhakikisha barabara za Vijijini zinaboreshwa ili kuwezesha wananchi kusafirisha mazao yao kwa urahisi na kukuza uchumi wao.

''Tumekagua mradi huu hapa Kilolo na kujjionea kazi nzuri iliyofanywa na TARURA, mradi umekamilika na sasa wananchi watatumia muda mfupi kusafiri na kusafirisha mazao yao,” alisema Mhandisi Kabaka. 

Kwa upande wake Makamu Mweyekiti wa Bodi hiyo, Bibi Julieth Magambo amesema kuwa, uchumi wa wananchi unategemea barabara na hivyo Serikali itaendelea kuboresha barabara za Vijijini ili wananchi waweze kuzifikia buduma za Kijamnii kwa urahisi na kuboresha uchumi wao.

Aidha, alieleza kuwa ni jukumu la bodi kuzisimamia barabara hizo na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye ameamua kwa dhati kuhakikisha kuwa barabara za vijijini zinafunguka na kuwafikia wananchi ili ziwaunganishe na miji na kurahisisha usafiri na usafirishaji.

Naye Mkurugenzi wa Barabara TARURA, Mhandisi Venant Komba amesema kuwa TARURA inaendelea na ujenzi wa Barabara ikiwa ni pamoja na kufungua barabara mpya ili kuwezesha wananchi kuyafikia maeneo haliyokuwa hayafikiki. 

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa miwili inayotekeleza miradi ya ujenzi wa barabara za Lami “ Agri-Connect “ chini ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya.

Mradi huu unalenga kuwasaidia wakulima vijijini kuimarisha mnyororo wa thamani ya mazao yao hasa mazao ya chai,kahawa,mbogamboga na mazao mengine yanayohitaji kusafirishwa kwa haraka toka Mashambani hadi Viwandani na Sokoni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news