TEITI yawaongezea maarifa wananchi kuhusu rasilimali madini, mafuta na gesi asilia

NA MWANDISHI WETU

AFISA Mawasiliano wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Godwin Masabala amesema kuwa taasisi hiyo imedhamiria kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa namna inavyotimiza majukumu yake ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa mujibu wa sheria. 
Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Erick Ketagory (wa kwanza kulia) akiwa na afisa habari wa taasisi hiyo, Godwin Masabala wa pili kulia) wakizungumza na wageni waliotembelea kwenye banda lao kufahamu jinsi taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. 
Kamishna Msaidizi Tume ya Madini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa (FEMATA), Haroun Kinega (kulia) akitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kumaliza ziara yake fupi katika Banda hilo.Ameyataja majukumu yao wanayoyasimamia kwa mujibu wa sheria ni pamoja na kuweka wazi taarifa za Mapato ya Serikali na malipo ya Kodi yanayotoka kwenye Kampuni za Madini,Mafuta na Gesi Asilia kwa Umma ili kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali hizo. 

Masabala ameyasema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari yaliyofanyika Julai 11,2022 katika Banda lao lililopo ndani ya Banda kuu la STAMICO kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi Tume ya Madini Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wadogo wa madini (FEMATA) Haroun Kinega (kulia) akimsikiliza Afisa Msimamizi wa Fedha wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali madini, Mafuta na Gesi asilia (TEITI) Erick Ketagory (kushoto) alipokuwa katika Banda lao lililopo ndani ya banda kuu la STAMICO katika maonesho ya sabasaba leo Julai 11,2022 Jijini Dar es salaam.

Amefafanua kua Taasisi hiyo imeundwa kwa Sheria namba 23 ya TEITA ya mwaka 2015 ambayo imeunda Kamati ya Uwazi na Uwajibikaji (Kamati ya TEITI) yenye wajumbe nane(8) na inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu Ludovick Utouh na kazi za kila siku za TEITI zinatekelezwa na Katibu Mtendaji. 

“Taasisi hii ina wajibu mkubwa wa kuhamasisha Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini,Mafuta na Gesi Asilia,”amefafanua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news