'Tujitokeze kwa wingi na tusifiche umri wetu, tuhesabiwe kwa maendeleo yetu'

NA DENNIS GONDWE

WANANCHI wa Kata ya Majengo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakajayofanyika Agosti 23, 2022 ili kuiwezesha Serikali kuwaletea maendeleo.

Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Majengo, Shifaa Ibrahim alipotoa salamu wakati wa hitimisho la zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika Soko kuu la Majengo lililopo Kata ya Majengo jijini hapa.

"Mimi nipo tayari kuhesabiwa wewe je? Napenda kuwakumbusha ndugu zangu wote tarehe kuwa tarehe 23 Agosti, 2022 tuwe tayari kuhesabiwa. Naomba mwambie mwenzio mimi nipo tayari kuhesabiwa, mwenzangu je?. Tujitokeze kwa wingi tusifiche umri wetu, tuhesabiwe ili serikali yetu iweze kutusaidia kimaisha, kimapato na kimaendeleo”.

Kwa upande wake mfanyabiashara katika soko la Majengo, Safina Kessy alisema kuwa yupo tayari kwa zoezi la Sensa kutokana na hamasa aliyoipata.

Aidha, alipongeza zoezi la usafi kufanyika katika soko hilo. Masoko ni maeneo ambayo mara nyingi yanasahaulika katika kampeni za usafi na kufanya mazingira ya biashara kuwa magumi na kupoteza wateja.

Zoezi la usafi kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilifanyika katika Soko kuu la Majengo likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news