RAIS MUSEVENI WA UGANDA NA RAIS NDAYISHIMIYE WA BURUNDI WAONDOKA NCHINI,WAZIRI MKENDA AWAAGA

NA MATHIAS CANAL

RAIS wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Rais wa Burundi Mhe Evariste Ndayishimiye leo tarehe 23 Julai 2022 kwa nyakati tofauti wameondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuagwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda.
Viongozi hao waliwasili nchini tarehe 21 Julai 2022 ambapo wameshiriki kwenye Mkutano wa 22 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kuanzia tarehe 21-22 Julai 2022 katika Ukumbi wa kimataifa wa mikutano-AICC Jijini Arusha.
Kadhalika, viongozi hao waliungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe Uhuru Muigai Kenyatta, katika ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news