Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Julai 26,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2768.31 na kuuzwa kwa shilingi 2796.92 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 9.55 na kuuzwa kwa shilingi 10.11.
Hayo ni kwa mujibu wa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Julai 26, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 339.94 na kuuzwa kwa shilingi 343.21 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 16.81 na kuuzwa kwa shilingi 16.98.

Franka ya Burundi (BIF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) ikinunuliwa kwa shilingi 624.29 na kuuzwa kwa shilingi 630.49.

Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.27 huku shilingi ya Uganda (UGX) ikinunuliwa kwa shilingi 0.57 na kuuzwa kwa shilingi 0.60.

Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 136.83 na kuuzwa kwa shilingi 138.15 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.34 na kuuzwa kwa shilingi 19.27.
Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2348.47 na kuuzwa kwa shilingi 2372.88 huku Dola ya Marekani (USD) inanunuliwa kwa shilingi 2282.98 na kuuzwa kwa shilingi 2315.91.

Post a Comment

0 Comments