Wananchi wafurika banda la Benki Kuu katika Maonesho ya Sabasaba


Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji BoT, Bw. Kened Nyoni, akizungumza na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Kibasila walipotembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina. 
Mchambuzi wa Masuala ya Fedha BoT, Bw. Ephraim Madembwe, akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Dhamana za Serikali kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bi. Restituta Minja, akitoa elimu ya namna ya kutambua Alama za Usalama katika noti zetu kwa mwananchi alietembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Mkaguzi wa Mabenki BoT, Bw. Faridi Masasi, akielezea jambo kuhusu namna BoT inasimamia Sekta ya Fedha nchini kwa mwananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Meneja, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Victoria Msina, akitoa elimu kuhusu historia ya noti zilizochapishwa na BoT mwaka 1977 kwa mwananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Wananchi mbalimbali wakiwa katika banda la BoT kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) kwa ajili ya kupata elimu kuhusu kazi na majukumu ya BoT. 
Mchumi Mwandamizi BoT, Bi. Anjelina Mhoja na Bw. John Mero, wakitoa elimu kuhusu uchumi wa Tanzania kwa mwananchi waliotembelea banda la BoT katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mkuu Mwandamizi wa Benki, Bi. Joyce Njau akitoa elimu kuhusu namna BoT inasimamia Mifumo ya Malipo ya Taifa nchini kwa mwananchi alietembelea banda la BoT katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam. (Picha na BoT).

Post a Comment

0 Comments