Waziri Dkt.Ndumbaro ateta na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amefanya mazungumzo na Bi. Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya masuala ya haki za binadamu ikiwemo kutolea ufafanuzi tuhuma kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na Hifadhi ya Ngorongoro. Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 15 Julai 2022, Geneva Uswisi.
Kwa upande wake, Bi. Bachelet ameshukuru na kupongeza kwa namna ambavyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotekeleza masuala ya haki za binadamu hususan chini ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika mkutano huo, Dkt. Ndumbaro aliambatana na Mhe. Maimuna Tarishi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Geneva na Mhe. Hoyce Temu, Balozi na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Geneva.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news