Halmashauri zavunja rekodi ya miaka 10 ukusanyaji mapato 2021/22

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhesshimiwa Innocent Bashungwa amesema kuwa, katika kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2022 halmashauri nchini zimekusanya Shilingi Bilioni 888.7 ambayo ni asilimia 103 ya makisio ya mwaka husika.
Ameyasema hayo leo Agosti 2, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mapato na matumizi ya ndani ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Mheshimiwa Bashungwa amesema kuwa, katika mwaka wa fedha 2021/22, halmashauri zilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 863.9 kutoka kwenye vyanzo vya mapato ya ndani.

“Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Juni 2022, Halmashauri zimekusanya Shilingi Bilioni 888.7 ambayo ni asilimia 103 ya makisio ya mwaka husika.

“Uchambuzi wa taarifa za mapato ya ndani ya halmashauri katika mwaka wa fedha 2021/22, unaonesha kuwepo kwa ongezeko la mapato halisi yaliyokusanywa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 131.7, ikilinganishwa na kiasi halisi kilichokusanywa katika mwaka wa fedha 2020/21, cha Shilingi Bilioni 757.1, sawa na ongezeko la asilimia 17,”amesema Mheshimiwa Bashungwa.

Amesema, kiwango hicho hakijawahi kufikiwa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, kwani Halmashauri hazijawahi kufikia malengo yao ya mwaka kwa asilimia 100.

HALI YA MAKUSANYO YA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA MIAKA 10 MFULULIZO KUANZIA MWAKA 2012-2013 HADI MWAKA 2021/2022


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news