Je? Sensa Agosti 23, ina umuhimu wowote katika maisha yangu

NA DIRAMAKINI

NDIYO. Kwa nini? Kwa sababu Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum.

Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) inasema kuwa, takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.

Mimi na familia yangu, tupo tayari kuhesabiwa Agosti 23, 2022 wewe pia jiandae kuhesabiwa Agosti 23 na kuhakikisha unatoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa ili kuiwezesha Serikali kutimiza majukumu yake ya kuandaa mipango ya maendeleo kwa ustawi bora wa Taifa na Watanzania wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news