Kazi ni heshima ya mtu, hivyo tuifanye kwa bidii kujiletea maendeleo-Waziri Simbachawene

NA MWANDISHI WETU

WAKRISTO nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujietea maendeleo, changia pato la Taifa na kutatua changamoto zilizo katika maeneo yao.
Picha ya pamoja baada ya ibada ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati akizunguma katika sherehe ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma baada ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Askofu Donald Mtetemela kumaliza muda wake.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa Sherehe za kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.Waziri Simbachawene alisema chanamoto nyngi za kiuchumi katika jamii zitatauliwa endapo wananchi watajituma kufanya kazi na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali kama ambavyo maandiko matakatifu yanaagiza watu kufanya kazi.

“Lazima wakristo wa sasa tufanye kazi lazima tutae changamoto kwenye maeneo yetu maana imeandikwa katika biblia asiyefanya kazi na asile kwahiyo kufanya kazi ndio uhai wako, heshima yako na ukizalisha utaweza kuendesha maisha yako binfasi, utashiriki katika kazi ya Mungu na Taifa zima,” alisema Waziri Simbachawene.
Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa Jijini Dodoma. Rev. George Chiteto (aliyelala) akiwekwa wakfu kuwa Askofu wa kanisa hilo.Pia aliongeza kwamba serikalii itaendelea kushirikiana na taasisi za dini kwani zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo, kusimamia maadili na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya watu wasiyo na hofu ya Mungu.

“Licha ya mchango mkubwa wa kanisa hili kwa serikali lakini kumekuwa na mmomonyoko wa maadili, magonjwa na majanga mbalimbali hivyo ni muhimu kushirikiana na serikali ili kuokoa vijana na watoto wetu na ni matumaini yetu viongozi wa dini mkiendelea kusimama imara na kutoa huduma ya kiroho tutatatua changamoto hii,” alieleza.
Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo Mndolwa akifafanua jambo wakati wa ibada ya kumweka wakfu Askofu wa tatu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Rev. George Chiteto iliyofanyika Jijini Dodoma.

Aidha alibainisha kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua za kisheria kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa , ufisadi, utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma pamoja na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Mhashamu Dr. Maimbo Mndolwa aliipongeza serikali kwa kuwa mstari wa mbele kuziunga mkono taasisi za dini katika nyanja zote huku akimtaka Askofu Chiteto kufanya kazi kwa kumtegemea Mungu hatimaye kufikia malengo ya kanisa.

Baadhi ya waumini wakifuatilia matukio mbalimbali katika ibada hiyo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule alitoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutumia fursa ya serikali kushusha bei ya mbolea kwa kujikita katika kilimo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news