Magu yatafuta mwarobaini wa changamoto ya wafugaji katika Hifadhi ya Sayaka

NA HAPPINESS SHAYO

MKUU wa Wilaya ya Magu, Mhe. Salum Kali amekutana na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya hiyo kujadili mikakati ya kutatua changamoto ya wafugaji katika Hifadhi ya Sayaka Wilaya ya Magu.
Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Magu. Mhe.Kali amesema moja ya mwarobaini wa tatizo hilo ni kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuzuia wananchi kuingiza mifugo hiyo hifadhini.
Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe Mary Masanja amesema, suala la uvamizi wa Hifadhi ya Sayaka linatakiwa kutatuliwa kwa kushirikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news