Rais Samia atoa maagizo Wizara ya Fedha,OR-TAMISEMI

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na TAMISEMI kupitia Halmashauri zote nchini na kuhakikisha zinaweka mipango ya kukusanya mapato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi Barabara ya Chunya-Makongorosi kilomita 39 iliyojengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Matundasi Chunya Mkoani Mbeya.

Rais Samia amesema hayo katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Chunya -Makongorosi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 39 iliyofanyika katika uwanja wa Matundasi.

Aidha, Rais Samia amesema mapato yanayokusanywa na Halmashauri yakisimamiwa vizuri yanaweza kujenga miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Akizungumza na wananchi wa Chunya mjini, Rais Samia ameagiza Madiwani na Wenyeviti wa eneo hilo wanaopata mapato mengi kutokana na kutoa leseni nyingi za biashara kujenga kituo cha mabasi cha Chunya.

Vile vile, Rais Samia ameeleza barabara hiyo itafungua fursa za kibiashara kwa wananchi wa Chunya kwani inaunganisha mkoa wa Mbeya na mikoa ya jirani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news