Mchungaji mbaroni kwa tuhuma za kumlawiti mtoto Shinyanga

NA DIRAMAKINI

MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Makedonia Kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga jina limehifadhiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka nane.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amebainisha hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari Agosti 12, 2022.

Alisema, Jeshi hilo la Polisi lilipata taarifa juu ya Mchungaji huyo, kuwa huwa ana mlawiti mtoto huyo wa miaka nane (jina limehifadhiwa) ndipo wakamkamata na wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika hatua nyingine za kisheria zitachukua mkondo wake.

“Jeshi la Polisi hapa Shinyanga tunamshikilia Mchungaji wa Kanisa la KKKT kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka nane majina yao tumeyahifadhi kwa ajili ya uchunguzi, na utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,”amesema Kamanda Magomi.

Post a Comment

0 Comments