NIC yatambulisha bima ya mazao kwa wadau wa kilimo

NA HUGHES DUGILO

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) limetumia Shilingi milioni 500 kama malipo ya Bima ya Mazao kwa wakulima waliopatwa na majanga yaliyopelekea kuharibika kwa mazao yao shambani.

Akizungumza Agosti 1,2022 katika Maonesho Nanenane yanayofanyika Kitaifa jijini mbeya, Meneja wa NIC Mkoa wa Mbeya, Justine Seni amesema kuwa, wakulima na wafugaji wamenufaika na bidhaa hiyo toka ilipoingizwa sokoni na kwamba shirika linaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wadau katika sekta ya kilimo na mifugo kutumia fursa ya uwepo wa Bima hiyo na kujiunga nayo ili kujihakikishia usalama wa mazao yao.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Mbeya Justine Seni (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Shirika hilo kwenye Banda lao katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
Wakala wa Bima wa NIC Chrisostme Haule ((kulia) akimuhudumia Mteja aliyefika kupata huduma za Bima kwenye Maonesho hayo.
Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Mbeya Justine Seni (kushoto) akiwa na Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa Shirika hilo Alex Suzuguye (kulia) wakifurahia jambo katika Banda lao.
Afisa Uhusiano wa NIC Ephrasia Mawalla akizungumza na Mwandishi wa Habari (hayumo pichani) aliyetembelea kwenye Banda lao kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo kwenye Katika Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya. (PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO).

“Bima hii ya kilimo kwa sasa inafanya vizuri sana sokoni toka tulipoianzisha imekuwa ni msaada kwa wakulima wetu na wafugaji na tayari tumeshatoa zaidi ya Milioni 500 kwa mwaka uliopita. Hapa nanenae tumekuja kushiriki lakini pamoja na mambo mengine pia tunaendelea kuiuza hii bidhaa ili wakulima wengi wapate kujiunga na kupata uhakika wa usalama wa mazao yao” amesema Seni.

Ameainisha maeneo ambayo mkulima anaweza kunufaika na Bima hiyo ni pamoja na ukame, mafuriko, magonjwa na wadudu wasiodhibitika au kutibika, vimbunga na Mvua ya mawe. Pia amesema kuwa Shirika litaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo na mifugo kuhakikisha malipo ya fidia zao yanapatikana kwa haraka kama ilivyo kawaida ya Shirika hilo katika kulipa waathirika wa majanga mbalimbali.

Naye Afisa maendeleo ya Biashara Mwandamizi wa NIC Alex Suzuguye amesema kuwa Shirika hilo limefanikiwa kuwafikia wakulima zaidi ya 500 waliojunga na Bima hiyo na kwamba vipo vyama vya Ushirika zaidi ya 200 vilivyopo katika mikoa mbalimbali ambavyo wakulima wao pamoja na wafugaji wamejiunga na Bima hiyo.

Aidha amesema kuwa wakulima walionufaika na Bima hiyo ni pamoja na wakulima wa Mpunga katika Mkoa wa Mbeya, wakulima wa Mpunga na Miwa katika Mkoa wa Morogoro, wakulima wa Korosho katika mikoa ya Kusini, na mazao mengine yanayozalishwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

“Sisi kama Bima tumeendelea kutoa huduma hii na kwakua ni Shirika la Serikali ndio tumepewa dhamana ya kuhakikisha wakulima wetu mazao yao wanalindwa na kwamba kilimo chao kiwe chenye tija wasipate hasara pale wanapopatwa na matatizo” ameongeza Suzuguye. Na kuongeza kuwa.

“Mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wote na wafugaji waliojiunga na Bima hii, wamekuwa wakiipongeza Serikali na Shirika lao kwa kuanzisha Bima hii” ameongeza.  Huduma hii na kwakua ni Shirika la Serikali ndio tumepewa dhamana ya kuhakikisha wakulima wetu mazao yao wanalindwa na kwamba kilimo chao kiwe chenye tija wasipate hasara pale wanapopatwa na matatizo” ameongeza Suzuguye. Na kuongeza kuwa.

“Mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wote na wafugaji waliojiunga na Bima hii, wamekuwa wakiipongeza Serikali na Shirika lao kwa kuanzisha Bima hii” ameongeza Suzuguye. Na kuongeza kuwa

“Mpaka sasa hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wakulima wote na wafugaji waliojiunga na Bima hii, wamekuwa wakiipongeza Serikali na Shirika lao kwa kuanzisha Bima hii” ameongez.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news