Rais Dkt.Mwinyi ateta na Balozi wa Amani Duniani

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Kiongozi wa Kiroho na Balozi wa Amani Duniani,Gurudev Sri Sri Ravi Shankar pamoja na ujumbe wake jijini Ikulu Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa Amani Duniani, Gurudev Sri Sri Ravishankar (kulia kwa Rais) kutoka Bangalore nchini India akiwa na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar leo Agosti 26, 2022.

Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine Rais Dkt.Mwinyi alimueleza kiongozi huyo utayari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kufanyakazi nae, ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo vijana na kusema Zanzibar ina vijana wengi wasio na ajira, ambapo kimsingi wanahitaji kujengewa uwezo ili waweze kufanya kazi.

Aidha, amesema Zanzibar ni kisiwa chenye utajiri mkubwa wa kuwa na viungo mbalimbali, ambapo pia hutumika kwa ajili ya tiba asilia na kubainisha eneo hilo kuwa muhimu katika kuendeleza ushirikiano.

Naye Kiongozi wa kiroho na Balozi wa Amani Duniani, Geredev Sri Sri Rav Shankar amesisitiza umuhimu wa mani katika jamii pamoja na kubainisha programu inayohusiana na tiba asilia ambayo itaendeshwa katika nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania.

Post a Comment

0 Comments