Rais Dkt.Mwinyi awapongeza Waumini wa Msikiti wa Masjid Nabaw kwa kushiriki masuala mbalimbali ya kijamii

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza waumini wa Msikiti wa Masjid Nabawi uliopo maeneo ya Mbuyu Mnene, Mkoa Mjini Magharibi kwa kuwa mfano mwema katika kushiriki masuala mbalimbali ya kijamii.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Kiislam katika kuitikia dua ikisomwa na Sheikh Ali Mohammed Ali.(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid Nabawi Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B”Unguja leo Dkt.Mwinyi ametoa pongezi hizo katika salamu zake kwa waislamu wa msikiti huo baada ya kukamilisha Ibada ya sala ya Ijumaa.

Amesema, waumini wa msikiti huo wamekuwa wa kwanza kutekeleza kwa vitendo yale aliyokuwa akiyahubiri katika msikiti mbalimbali, juu ya umuhimu wa waislamu kushikiri katika masuala ya kijamii, kama vile kusaidia yatima, wajane, walemavu, wenye mahitaji pamoja na kusimamia usalama wa maeneo yao.

Amesema, hatua ya waumini wa msikiti huo kutoa hundi ya shilingi 500, 000 kwa serikali ili kusaidia huduma nyingine za maendeleo au kijamii, ni za kupongezwa na mfano mwema.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Masjid Nabawi Mbuyu Mnene Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Masjid hiyo leoAlielezea kuwa mchango huo aliokabidhiwa na uongozi wa msikiti huo sio mdogo na kusema utasaidia maeneo mengine yenye mahitaji.

Aidha, amewataka wananchi kote nchini kuwa na subira wakati huu wakisubiri makarani wa sensa wapite katika maeneo yao na kukamilisha zoezi la kuhesabu watu ili Serikali iweze kupanga mipango yake ya maendeleo.

Naye Katibu Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume alisema sensa ni sunna kwa sababu Mtume Muhammad (SAW) yeye mwenyewe alifanya sensa kwa kutaka kutambua idadi ya watu walioingia katika Dini hiyo, hivyo akatoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika zoezi hilo linaloendelea kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mapema, Imamu wa Msikiti huo Sheikh Ali Aboud alisema msikiti huo umekuwa kiunganishi kikubwa cha watu na kubainisha namna wananchi wanavyoishi vyema kama ndugu pamoja na kushirikiana katika masuala mbali mbali, yakiwemo ya kijamii.

Alitoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Mwinyi kwa kufika msikitini hapo na kuswali pamoja na waumini wa msikiti huo, ambapo kwa muda mrefu walisubiri jambo hilo.

Aidha, Katibu katika sala hiyo ya Ijumaa Sheikh Suleiman aliwataka waislamu kuzingatia wakati ili kufikia malengo yao katika maendeleo ya dunia na akhera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news