Rais Samia amuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, majaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza (SACP) Mzee Ramadhani Nyamka Cheo kipya cha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) kabla ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka kuwa Mkuu wa Jeshi hilo katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Majaji wa Mahakama Kuu kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Majaji wa Mahakama Kuu pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka wakila kiapo cha Maadili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Majaji wa Mahakama Kuu pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka wakiweka Saini kwenye viapo vyao vya Maadili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali mara baada ya kumuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka pamoja na Majaji Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango, Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu aliowaapisha Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) Mzee Ramadhani Nyamka mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 29 Agosti, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news