'Serikali imeonesha nia njema mchakato mabadiliko ya Sheria za Habari nchini'

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) ambaye pia ni wakili wa kujitegemea na mwakilishi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), James Marenga amesema kuwa, katika mchakato wa mabadiliko ya Sheria za Habari,Serikali imeonesha nia ya kufanyia kazi vipengele mbalimbali hivyo mchakato huo utapata majibu yatakayomaliza kiu sekta ya habari.
Wakili huyo ameyasema hayo Agosti 27, 2022 katika Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa na Star TV ya jijini Mwanza.

Amesema kuwa, nia ya Serikali ni kuhakikisha mwafaka unapatikana katika Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria ya Habari na wadau wa habari wamekiri kuwepo kwa nia hiyo.

“Kwa hatua hii tunaona kuwa Serikali imeonesha nia katika kuhakikisha kuwa mabadiliko yua sheria ya habari yanafanyikiwa kazi na kupata mwafaka wa vipengele vya Sheria ya Habari vyenye ukakasi inaonekana wazi,” amesema Wakili Marenga.

Wadau wa habari wamekuwa wakilenga vifungu vinavyotisha waandishi na uhai wa tasnia ya habari nchini na kwamba, sio sheria yote ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 havifai.

“Kabla ya kuwapo kwa sheria hiyo, kulikuwa na sheria ya mwaka 1976 ambayo ilikuwa na changamoto kubwa sana ya udhibiti na uchapishaji.Sheria hiyo ilikuwa ikimpa mamlaka makubwa sana Waziri wa Habari kudhibiti uchapishaji wa magazeti,”amesema Marenga.

Amesema kwamba, mamlaka hayo kwa waziri, sheria mpya ilipotungwa (Sheria ya Huduma za Habari ya 2016) ikayahamisha na kuyapeleka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambapo sasa anaweza kufunga magazeti, kunyima leseni wanahabari na hata kutoa hukumu kwa vyombo vya habari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news