Tanzania yaihakikishia Iran mazingira salama ya biashara na uwekezaji

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mazingira salama ya biashara na uwekezaji.
Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) amebainisha hayo alipofungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mbarouk amesema Tanzania imejitahidi kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza nchini.

“Tunapoendelea na juhudi za kuimarisha mazingira ya biashara na kukuza uwekezaji nchini Tanzania, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wawekezaji zaidi kutoka Iran kuwekeza nchini Tanzania. Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu na iliyojaliwa kuwa na maliasili nyingi hasa katika maeneo ya kimkakati yakiwemo Mafuta na Gesi, Madini, Viwanda, Utalii, Uchumi wa Bluu, Kilimo na Mifugo,” alisema Balozi Mbarouk.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Amir Abdollahian akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk walipokutana kwenye ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian amesema kupitia kongamano hilo la biashara na uwekezaji, litatoa fursa kwa wafanyabiashara alioambatana na kujionea fursa mbalimbali zinazopatikana Tanzania.

Aidha, Mhe. Abdollahian amekiri kuwa Tanzania ina fursa nyingi zinazohamasisha na kuvutia biashara na uwekezaji. “tumeridhishwa na juhudi za Serikali ya Tanzania za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na tunaahidi kuwa tutaendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kutoka Iran kuja kuwekeza Tanzania,” amesema Mhe. Abdollahian.

Post a Comment

0 Comments