TANZIA:Mwenyekiti wa TLP, Dkt.Augustino Lyatonga Mrema afariki

NA DIRAMAKINI

MWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Buberwa Aligaesha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo Jumapili Agosti 21,2022 saa 12:15.

Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro na amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news