'Tupo tayari kuhesabiwa Agosti 23 na kutoa taarifa sahihi kwa makarani'

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepanga kufanya Sensa ya Watu na Makazi ifikapo mwezi Agosti 2022.

Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), ipo kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya kufanya sensa hiyo.

Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012.

Hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012. Kumbuka kila Mtanzania kwa sasa yupo tayari kuhesabiwa, wewe je? Jiandae kuhesabiwa Agosti 23; "Watanzania tupo tayari kuhesabiwa wote na kutoa taarifa sahihi kwa makarani".

Post a Comment

0 Comments