Watendaji wa Sensa watakiwa kufanya kazi kwa bidii

NA MWANDISHI WETU

WATENDAJI wa Sensa wapewa wito kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukamilisha kwa ufanisi zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022. 
 
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika Ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es saalam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere convection Centre, Dar es saalam. (Picha na OWM).

“Baada ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kuna kazi kubwa ya mchakato, lazima tuwe tayari kusimama pamoja na kufanya kazi usiku na mchana ili zoezi liweze kukamilika,"amesema.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dkt.John Antony Jingu akizungumza katika kikao cha saba cha kamati kuu ya Taifa Sensa ya Watu na Makazi 2022 kilichofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convection Centre, Dar es salam.
 
Waziri Simbachawene ameipongeza kamati ya Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 kwa kufanya kazi zake vizuri na hivyo kufanikisha maamuzi ya kamati kuu ya Taifa ya Sensa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Bw.Kaspar Mmuya akizungumza jambo kabla ya kikao na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt, Alibina Chuwa.

“Vilevile napongeza Wizara zote, Wadau wa Maendeleo na Sekta binafsi kwa ushirikiano mkubwa walioonesha wakati wote wa maandalizi ya sensa ya watu na makazi,"amesema.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt, Alibina Chuwa amesema kwa wakuu wa kaya ambao hawatakuwa nyumbani wameandaa fomu maalumu ambayo itakuwa na maswali 11 ambayo itasambazwa kwa wakuu wote wa kaya kupitia kwa makarani wao wa sensa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (OR-TAMISEMI), Prof.Riziki Shemdoe kabla ya kikao.

“Wakuu wa kaya waandike taarifa za watu ambao watakuwa wamelala usiku wa kuamkia siku ya sensa ili kumrahisishia karani kujaza taarifa kwenye kishikwambi atakapofika kuchukua taarifa,"amesema.

Post a Comment

0 Comments