Waziri Bashungwa abadilishana mawazo na wajasiriamali mitaani

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa leo ametembelea wafanyabiashara wadogo na wauza vyakula na kuteta nao kwenye maeneo tofauti ya Mji wa Kayanga Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera.




Katika matembezi hayo, Waziri Bashungwa amesikiliza mapendekezo na maoni yao juu ya hatua ambazo serikali inaendelea kuzichukua kwa kuboresha mazingira ya wafanyabiashara hao nchini.

Maeneo aliyotembelea Waziri Bashungwa ni pamoja na Soko la Wafanyabiashara wadogo eneo la Mabatini, wauza vyakula na wauza nguo za mitumba katika mitaa tofauti ya Mji wa Kayanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news