Waziri Bashungwa: Tupo tayari kufia 'site' kuliko kumuangusha Rais Samia

NA OR- TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Innocent Bashungwa amesema wako tayari kuifia 'site' kuliko kumuangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi na kusimamia utekeleza miradi ya maendeleo.
Mhe. Bashungwa ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaa baada ya kuapishwa kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa na kusisitiza kwenda kujipanga, kubadilika na kuwa wizara inayowahudumia wananchi na inayotatua kero na changamoto za wananchi kwa wakati.
Amesema, asilimia 70 ya watumishi wa umma wako Ofisi ya Rais-TAMISEMI na kuwa kila mmoja akitekeleza wajibu wake inamaana utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi itatekelezwa kwa zaidi ya asilimia 70.

Amesema, kwa mwaka 2022/23,Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeweza kukusanya mapato na kuvuka malengo kwa kukusanya mapato kwa asilimia 103 na kusisitiza kuwa bado kuna fursa kubwa ya kuongeza malengo hayo.
" Mheshimwa Rais umetuelekeza tuhakikishe tunadhibiti mianya yote ya upotevu wa mapato, timu hii iliyopo mbele yako mara baada ya kuapa, tunakwenda kujipanga na tunataka dhamira yako (Rais Samia) ya kuwahudumia wananchi kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI ikatimie, tuko tayari kufia site kuliko kukuangusha."

Aidha, Bashungwa alimuahidi Rais kuwa timu hiyo wataekenda kutekeleza maagizo anayoyato ikiwamo ya ukusanyaji mapato na kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za miradi.
"Nikuhakikishie Mheshimwa Rais hii ndio timu yako ya ushindi, umetuamini hatutakuangusha,"ameongoza Mheshimiwa Waziri.

Pia aliwakumbusha wakuu wa mikoa kujipanga kuhakikisha Sensa ya Watu na Makazi inafanyika kwa mafanikio.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news