KCCA yatwaa ubingwa Cambbiasso U20 Tournament dhidi ya Azam FC

NA DIRAMAKINI

TIMU ya KCCA ya Uganda imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Cambbiasso U20 Tournament.
Ni baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC uliopatikana jana katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Mtanage huo ambao dakika 90 za awali zilikata kwa pande zote kuambulia matokeo bila bila, waliongezewa zingine ambazo KCCA ilionekana walishatambua madhaifu ya wenyeji wao.

Zikiwa zimesalia dakika tatu muda wa nyongeza kumalizika, Abubakar Mayanja alifunga bao na kuipa timu yake ushindi ambao uliwapa raha Waganda.

Ni baada ya kosa la awali la Ally Hassan kugonga mwamba wa goli, mshambuliaji huyo wa KCCA aliusoma mchezo hivyo kutupa jalo moja hadi kwenye nyavu za Azam.

Kabla ya bao lao la KCCA, Azam ambao walitumia muda mwingi kwenye safu ya ulinzi, walipata nafasi adimu ya kushinda mchezo huo, lakini Clement Kabela alishindwa kufanya jambo.

Post a Comment

0 Comments