Waziri Prof.Mkenda autaka uongozi Wilaya ya Rungwe kutenga eneo mapema ujenzi Chuo cha VETA

NA MATHIAS CANAL-WEST

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kutafuta eneo la zaidi ya hekari 20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA).
Waziri Mkenda ameyasema hayo leo Agosti 7, 2022 alipopewa fursa ya kujibu hoja zilizoibuka wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wilayani Rungwe ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mbeya iliyoanza tarehe 5 Agosti 2022 hadi tarehe 8 Agosti 2022.
Waziri Mkenda amesema kuwa Katika bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 zimetengwa shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi stadi-VETA katika wilaya mbalimbali nchini hivyo Wilaya ya Rungwe ni mojawapo katika mpango huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news