ACHANA NA MATOKEO:Shughuli ya Yanga SC ilinoga namna hii

NA DIRAMAKINI

LICHA ya wenyeji Yanga SC kuchapwa mabao 2-0 na mabingwa wa Uganda katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha Siku ya Mwananchi na kwa ujumla Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dares Salaam,maandalizi na namna ya upangiliaji wa shughuli hiyo ulionekana kufana zaidi.
Mabao yaliyowazamisha nyumbani mabingwa wa Tanzania yalifungwa na Milton Karisa dakika ya kwanza tu na Anukani Bright dakika ya 64.
Hata hivyo, baada ya matokeo ya Agosti 6, 2022 Kikosi cha Yanga kinarejea kambini, Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao, Simba Agosti 13, 2022 katika dimba hilo.

Post a Comment

0 Comments