APNAC yaahidi ushirikiano kwa TAKUKURU kutokomeza rushwa

NA JAMES K.MWANAMYOTO

MAKAMU Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC), Mhe. Cecilia Pareso (Mb) amesema mtandao wao utashirikiana kikamilifu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwani rushwa inakwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) na baadhi ya watendaji wa TAKUKURU wakifuatilia mada ya wajibu wa wabunge wanachama wa APNAC Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa nchini iliyoandaliwa na TAKUKURU.

Mhe. Pareso amesema hayo jijini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) ili waweze kushirikiana vema na TAKUKURU katika kuitokomeza rushwa nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) Mhe. Cecilia Pareso (Mb) akizungumza wakati wa semina kuhusu elimu ya mapambano dhidi ya rushwa iliyoandaliwa na TAKUKURU jijini Dodoma kwa lengo kuwajengea uwezo wajumbe wa mtandao wa APNAC ili waweze kushirikiana vema na TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.

“Sisi wabunge ambao ni wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania kwa pamoja tunaunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha rushwa inatokomezwa nchini kwa sababu kukiwa na rushwa wananchi hawawezi kupata huduma wanayostahili,” Mhe. Pareso amesisitiza.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania, Mhe. Vita Kawawa (Mb) akieleza umuhimu wa semina waliyopatiwa na TAKUKURU katika kuwezesha utekelezaji wa majukumu yao pamoja na ushiriki wao katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini.

Naye, Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania, Mhe. Vita Kawawa (Mb) amesema semina waliyopatiwa imekuja wakati muafaka kwani itawawezesha kupata elimu ya kutosha ya jinsi ya kushirikiana na TAKUKURU katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma TAKUKURU Bw. Joseph Mwaiswelo akiwasilisha mada ya wajibu wa Wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) katika kuzuia vitendo vya rushwa nchini.

Mhe. Vita Kawawa amesema kuwa, semina waliyopatiwa itakuwa na manufaa kwa waheshimiwa wabunge ambao ni wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania, kwa sababu wanatoka katika maeneo ambayo fedha nyingi za miradi zimeelekezwa na Serikali, hivyo watatumia elimu waliyoipata kuzuia mianya ya rushwa ambayo inaweza kukwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifungua semina kuhusu elimu ya mapambano dhidi ya rushwa iliyoandaliwa na TAKUKURU kwa lengo kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kushirikiana na TAKUKURU katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa nchini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo wajumbe wa APNAC wakimuunga mkono kupambana na rushwa kwa kushirikiana na TAKUKURU watawezesha fedha za miradi kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, anaamini baada ya wajumbe hao wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania kupatiwa semina hiyo ya kuwawezesha kupambana na vitendo vya rushwa, watakuwa na ari na nguvu zaidi ya kukemea vitendo vya rushwa katika jamii inayowazunguka ikizingatiwa kwamba, wajumbe hao ni wajumbe wa kamati za fedha katika halmashauri zao.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni akieleza lengo la TAKUKURU kuandaa semina kwa wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) iliyofanyika jijini Dodoma.

Akizungumza kuhusu lengo la TAKUKURU kuandaa semina hiyo kwa wajumbe wa APNAC, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni amewaomba wajumbe wa APNAC kusaidia kuwahamasisha waheshimiwa wabunge wengine kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wananchi pindi wanapokutana nao katika mikutano na shughuli mbalimbali za kijamii.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) Mhe. Cecilia Pareso (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mtandao huo, mara baada ya kupata semina kuhusu elimu ya mapambano dhidi ya rushwa iliyoandaliwa na TAKUKURU jijini Dodoma.

Wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) kupitia Semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na TAKUKURU walipata fursa ya kupitishwa kwenye mada iliyohusu wajibu wao katika kuzuia vitendo vya rushwa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news