'Rushwa ni upofu, lazima tusimame imara kuishinda'

 MAKAMU Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC), Mhe. Cecilia Pareso (Mb) amesema mtandao wao utashirikiana kikamilifu na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwani rushwa inakwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Mhe. Pareso amesema hayo jijini Dodoma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania (APNAC) ili waweze kushirikiana vema na TAKUKURU katika kuitokomeza rushwa nchini.
 
“Sisi wabunge ambao ni wajumbe wa Mtandao wa Wabunge wa Kupambana na Rushwa Afrika tawi la Tanzania kwa pamoja tunaunga mkono juhudi za serikali kuhakikisha rushwa inatokomezwa nchini kwa sababu kukiwa na rushwa wananchi hawawezi kupata huduma wanayostahili,” Mhe. Pareso amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments