Balozi Possi ataja fursa zinazowafaa Watanzania nchini Ujerumani

NA DIRAMAKINI

BALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ujerumani, Mheshimiwa Dkt.Abdallah Saleh Possi tarehe 14, 2022 amezungumza na waandishi wa habari akiangazia mambo mbalimbali hususani diplomasia ya uchumi na fursa nyinginezo.
Mazungumzo hayo yamefanyika mubashara kupitia mtandao wa Zoom ambapo waandishi waliweza kushiriki moja kwa moja. Miongoni mwa yaliyosemwa na Balozi Possi ni pamoja na;

"Tumekuwa na ushirikiano wa kimaendeleo na nchi ya Ujerumani, Poland kwenye sekta ya maji, afya,nisharti na nyinginezo, mfano hivi karibuni serikali imemaliza kutekeleza miradi ya maji kwa ushirikiano na nchi ya Ujerumani kwenye miji kama Sumbawanga, Babati, Kigoma zaidi ya Euro milioni 20 kutumika.

Amesema, "Nchi ya Ujerumani na Tanzania imeshirikiana na serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Samia (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Jeshi iliyopo Dodoma ambayo hayati Rais Magufuli ndiye aliyeshuhudia utiaji saini baina ya nchi hizi mbili.

"Kipindi cha ugonjwa wa Uviko-19 nchi ya Ujerumani iliisaidia Tanzania fedha za kupambana na ugonjwa huu, sio tu kununua vifaa vya kujikinga bali hata kutoa mafunzo kwa madaktari wetu nyumbani namna ya kukabiliana na ugonjwa huu na kufanya utafiti wa namna ya kukabiliana nao.

"Kuhusu ulinzi na amani kumekuwa na wanajeshi wengi tu kutoka Tanzania kwenda Ujerumani kusomea masuala ya utawala bora kwa muda mrefu na Tanzania imekuwa ikishiriki kutuma wanajeshi wake kushiriki mission za kulinda amani katika jumuiya ya kimataifa.

"Moja ya fursa kubwa sana ambayo watanzania tunaweza kunufaika nayo kutoka Ujerumani, Poland, Peru ni soko kubwa la utalii, takwimu zinaonesha katika zile nchi zinazoleta watalii wengi zaidi kwa mwaka basi Poland na Ujerumani zimo.

"Ongezeko hili la watalii nchini limechagizwa na uwepo wa usafiri wa moja kwa moja kutoka Ujerumani kuja Tanzania na shirika la ndege la Euro Wings Discovery ambalo lilikuwa na safari ya kwanza kwenda Zanzibar sasa hivi litakuwa linaenda mpaka Arusha na Kilimanjaro.

"Kumekuwa na uhitaji mkubwa sana wa zao la kawaha nchini Ujerumani kutokana na hali yake ya hewa ni baridi hivyo hii ni moja ya fursa, Watanzania tuichangamkie.

"Kumekuwa na maonesho mbalimbali kama Ubalozi wa Ujerumani tukiyaanda kuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa wa kilimo na wateja kuona ni kwa namna gani wadau wa kilimo wanahusishwa katika upanuaji wa masoko, ndio maana sasa hivi zao kama parachichi limeshaanza kupatikana nchi ya Ujerumani kitu ambacho kilikuwa adimu kipindi cha nyuma.

"Biashara ya Tanzania na Ujerumani haijawa kubwa sana kama ile ya Tanzania na nchi za Asia, labda kutokana na vile vitu tunavyo-import na ku-export tunapata zaidi vitu vya kemikali na teknolojia na mitambo ya afya.

"Kupitia TIC na ZIPA tunaona mfano mpaka mwaka 2021 kupitia TIC miradi ya Ujerumani iliyokuwa imeandikishwa ni zaidi ya miradi 169 yenye thamani ya dola milioni 396 na zinakadiriwa kwamba miradi yote itatengeneza ajira 15,000.

"Kumekuwa na mikataba mbalimbali ya kielimu kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Ujerumani kupeleka wanafunzi Ujerumani kusomea masuala afya na kilimo;








Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news