Haji Manara avunja ukimya


"Nilivyokuwa Dodoma nilipata amani kubwa sana kuona viongozi wakubwa(Wabunge) wa pande zote yaani Simba na Yanga kupiga kelele bungeni wakati vikao vya bunge vikiendelea wakipaza sauti zao Haji manara achiwe huru.

"Binafsi nilifarijika sana jana viongozi wangu wa Yanga,,mwanasheria wangu walikutana na Viongozi wa Tff kujadili swala langu la kukata rufaa.Lakini cha ajabu leo nimepokea simu na msg Kutoka kwa watu watano ndani ya Tff wakinambia Haji rufaa yako haitaweza kufanikiwa kwani wamepanga kwenda kukazia hukumu yako Fifa kabisa.

"Kwa hali hii sasa tulipofikia sioni tena sababu ya kushindana na watu ambao wameapa kabisa kwa kusema lazima wanishushe hadhi yangu.Binafsi nimetengeneza jina langu Brandy yangu kwa gharama kubwa sana Sasa siwezi kukubali kuona taswira yangu inachafuliwa kisa mpira.

"Nipo Katika mazungumzo na familia yangu nataka niachane kabisa na mpira ili Mambo yangu mengine yaendelee.Najua Kuna watu wengi wanalipwa na watu ambao nawajua ili waandike tu habari za kunichafua mimi.

"Kuna watu hata nilivyokuja Yanga walijiapiza sitafanya kazi kwa Uhuru na Kama mnakumbuka Kwenye dabi yetu ya mwisho watu waliandika makala ya kunigombanisha na Yanga kwa kusema nimekwenda hotelini ambapo Simba waliweka kambi eti nimeenda kutoa siri.

"Sasa watu wamejiapiza Leo kwenda Fifa kukazia hukumu yangu ndio ujue watu wanataka kuona Haji manara anadondoka ili waje wafurahi.Napata amani sana kwa sasa haswa Kutoka kwa mashabiki wa Yanga kwa kuwa karibu nami kwa kunitia moyo na Viongozi wangu wanavyonipigania kurudi kazini.

"Binafsi sitawaacha kabisa Yanga hadi mwisho wa maisha yangu hapa duniani nitakuwa nao bega kwa bega hata Kama nitakaa pembeni na maswala ya football,"ameandika kwa kina Haji Manara.

Post a Comment

0 Comments