Hizi hapa bei mpya za mafuta nchini kote leo Septemba 7,2022

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli hapa nchini ambapo bei hizo zimeanza kutumika kuanzia leo Septemba 7, 2022.
Lengo ni kutaka wananchi wapate huduma bora bila kuwepo ongezeko litalofanya waumie katika kupata nishati hiyo hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Mhandisi Modestus Lumato, bidhaa za mafuta katika soko la Dunia za Julai 2022 zimepungua ikilinganishwa na bei hizo kwa Juni 2022.

"Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.

"Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, tarehe 7 Septemba 2022 (leo).Bei za Mafuta katika soko la dunia za Julai 2022 zimepungua ikilinganishwa na bei hizo kwa Juni 2022. Hivyo, bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua vilevile kwa kati ya shilingi 271/lita na shilingi 362/lita kwa petroli na kwa shilingi 430/lita kwa mafuta ya taa ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022.

Kwa mafuta ya dizeli, ukiiacha bei ya Tanga ambayo inashuka kwa shilingi 13/lita, bei za Septemba 2022 zimeongezeka kwa shilingi 37/lita na shilingi 86/lita kwa Dar es Salaam na Mtwara, sawia, ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022.

Ili kuendelea kupunguza madhara ya ongezeko la bei za dizeli hapa nchini ambapo shughuli nyingi za kiuchumi zinategemea dizeli na pia ili kupunguza tofauti kati ya bei za petroli na dizeli, Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 65 ili kupunguza bei za mafuta za mwezi Septemba 2022.

Kwa kutoa ruzuku hiyo, Serikali imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.

Jedwali Na.1 Bei za Mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kabla na baada ya ruzuku shilingi/lita
Kutokana na mgao wa ruzuku hiyo bei za Mafuta kuanzia tarehe 7 Septemba 2022 ni kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na.2.

Jedwali Na. 2 Bei za Mafuta za rejareja kuanzia tarehe 7 Septemba 2022-Shilingi/Lita
(a) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.

(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko.

EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.

(c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.

(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.

Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.

(e) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.

Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.

(f) Wauzaji wa Mafuta ya petroli wa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 3. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili

(g) Wauzaji wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 4.

Isipokuwa kwa wateja ambao wana msamaha wa kodi. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

JEDWALI 3: BEI KIKOMO ZA REJAREJA (SHS./LITA)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news