Makamishna wasaidizi wa ardhi wakalia kuti kavu

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mheshimiwa Dkt. Angeline Mabula amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt.Allan Kijazi kuhakikisha anaanza kuchukua hatua mara moja kwa makamishna wasaidizi wa ardhi walioshindwa kukidhi matarajio ya wizara pamoja na wasaidizi wao.
"Kama nilivyoeleza hapo awali mtiririko wa kazi zetu kama wizara unatuelekeza kada zote muhimu yaani zinazohusika na upangaji, upimaji, uthamini, umilikishaji na usajili kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano wa karibu.

"Ushirikiano huu sio ule wa kubembelezana, ni wa lazima kuutekeleza kwa kuwa umewekwa kisheria, vinginevyo hatuwezi kufikia kwa malengo tuliyojiwekea. Natambua Katibu Mkuu hili umelizungumza sana tangu ulipofika
wizarani na nimeanza kuyaona matokeo kwenye ngazi ya wizaa Makao Makuu. Tatizo bado lipo kwenye ngazi ya mikoa na halmashauri zetu.

"Huko kila mtu anafanya lake, muunganiko haupo na hali hiyo ndiyo inazorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi,ongezeko la migogoro na kushuka kwa tija kinyume na matarajio.Natambua Katibu Mkuu umefanyika uchambuzi wa kutosha kuhusu uwezo na udhaifu kwenye eneo la usimamzi na natambua tunaenda kuchukua hatua kuanzia leo.

"Sifurahishwi kabisa na utendaji wa baadhi ya Makamishna Wasidizi wa mikoa hasa wale wa mikoa ya Rukwa na Simiyu. Hili haliwahusu ninyi pekee, nataka ujumbe uwafikie wataalam wote wa sekta kuwa tutachukua hatua ili kuhakikisha tunaimarisha utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea;

Mheshimiwa Waziri Dkt.Mabula ameyabainisha hayo leo Septemba 6,2022 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi cha makamishna wa ardhi wasaidizi wa mikoa 26 nchini.

Pia amesema pamoja na hatua za kinidhamu ambazo zimechukuliwa kwa watumishi ikiwa ni pamoja na kuwaachisha kazi kwa mikoa ya Mbeya watatu na Dodoma wanne na ameagiza hatua zichukuliwe kwa mikoa mingine.

“Kwa mashauri ya kinidhamu ambayo yanaendelea, naelekeza yakamilishwe haraka. Mikoa ambayo tunakamilisha taratibu za kinidhamu kwa watumishi siku za hivi karibuni ni Mbeya, Dar es Saaam, Mwanza na Arusha na Lindi,"amesema Waziri Dkt.Mabula.

Mheshimiwa Dkt.Mabula amesema, wamebaini kuwa wapo watumishi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya udanganyifu kwenye zoezi la uthamini wa mali ambapo majina yao wameyapata na watachukua hatua za haraka.

“Siridhishwi kabisa na utendaji wa Mkurugenzi wa TEHAMA. Naelewa Katibu Mkuu analifanyia kazi; naelekeza lifanyiwe kazi kwa haraka na kwa muda mfupi,"amesema Mheshimiwa Waziri Dkt.Mabula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news