Mradi wa Kanda Maalum ya Kiuchumi ya Mkinga wazinduliwa, kuzalisha ajira 3,000 awamu ya kwanza

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe ameyashauri mashirika na kampuni za ndani na nje ya nchi yanayotaka kuwekeza nchini kuzingatia utunzaji wa mazingira kwa kutumia teknlojia za kisasa zitakazowezesha utunzaji wa mazingira ili kuvutia wawekezaji wengine zaidi.
Kigahe ameyasema hayo Septemba 27, 2022, jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kanda Maalum ya Kiuchumi ya Mkinga Mkoani Tanga unaotarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 3000 katika awamu ya kwanza.

Aidha, amewapongeza wawekezaji hao kwa kuziona fursa zilizopo mkoani Tanga na kisisitiza kuwa Serikali itawaunga mkono kwa kuwezesha uwekezaji huo kuwa na tija kwao na kwa Serikali kwa kuwa Sekta binafsi ni moja ya sehemu kubwa katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua.

"Serikali inatarajia uwekezaji huu kuwagusa moja kwa moja wananchi wa wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla kwani hiyo ndio itakuwa njia sahihi ya kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na hivo kuleta Tija katika uchumi wa Taifa,"amesema Kigahe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mkinga Special Economic Zone, Bw. Ally Kassim amesema lengo la mradi huo ni kutekeleza maagizo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha uwekezaji nchini unaongezeka ili kuleta usawa wa kiuchumi katika maeneo yatakayofanyiwa uwekezaji husika.

Aidha, amesema wawekezaji hao wamethibitisha kuwa hadi sasa jumla ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Brazil, Misri, Tunisia, Bulgaria, GCC, Ufilipino na India wameonyesha nia ya kuwekeza katika mradi huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Omary Mgumba amesema wawekezaji hao wamevutuwa na fursa mbalimbali ambazo ni Bandari, Bomba la mafuta pamoja na Ardhi yenye rutuba zinazowarahisishia kuapata malighafi na usafirishaji wa bidhaa na vitendea kazi kutoka ndani na nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news