Waziri Dkt.Kijaji atoa ushauri kwa wadau wa sekta ya nguo nchini

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amewashauri wadau wa sekta ya nguo kuainisha changamoto za kisera, kikodi na kiutendaji wanazokutana nazo ili azifanyie kazi.
Dkt.Kijaji ameyasema hayo Sepetemba 26, 2022 jijini Dodoma alipokutana na wadau wa sekta ya nguo na walio chini ya Chama cha Wazalishaji Nguo na Mavazi Tanzania (TEGAMAT) ili kujadili changamoto wanazokutana nazo.

Aidha, Waziri Dkt.Kijaji amewashauri wadau hao kutokufunga viwanda, kwa kuwa ni sekta inayotoa ajira nyingi kwa vijana.

"Njooni tukae tuongee, tupange kwa pamoja tuone cha kufanya, tunataka viwanda vifanye kazi katika Serikali ya Awamu ya Sita,"amesema Dkt.Kijaji.
Aidha ameongeza kuwa nia ya Serikali ni kuona viwanda nguo vya Tanzania vinakua shindani na vinahudumia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akiongea mbele ya Waziri Kijaji, Katibu Mtendaji wa TEGAMAT, Bw. Adam Zuku amesema vitenge vinavyoingizwa nchini kutoka nje ya nchi vinaumiza viwanda vya ndani vya nguo na ameomba kuwe na usimamizi wa hilo ili waweze kushindana katika soko la nje.
"Tunatamani kuhudumia soko la SADC,EAC, CFTA,"amesema Zuku.
Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wameiomba Serikali kuanzisha mitaala ya nguo kwa kuwa kwa sasa kuna uhaba wa wataalamu hao.

Pia wameiomba tozo zinazotozwa na taasisi mbalimbali za Serikali kujumuishwa kwa pamoja ili kuwapunguzia usumbufu na gharama kubwa za uendeshaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news