Rais Dkt.Mwinyi ashiriki maziko ya Askofu John Aukland Ramadhan

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Mwinyi ameshirki katika maziko ya Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Anglikana, John Aukland Ramadhan yaliofanyika Kanisa la Anglikana Mkunazini, Mkoa Mjini Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar leo. Maziko yamefanyika katika viwanja vya Kanisa la Anglikana Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu).

Katika hafla hiyo, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, wakiwemo Mawaziri kutoka SMZ na SMT, Waziri wa Nchi (OMPR) Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma alitoa salamu za rambirambi kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kusema wakati wa uhai wake Hayati Askofu John Ramadhan alitoa mchango mkubwa katika kuleta ustawi wa Taifa.
Amesema, Hayati Askofu Ramadhan alishirikiana kikamilifu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali katika kuhimiza na kusimamia amani nchini.

Waziri Hamza alisema, ana matumaini makubwa kuwa kanisa litayaendeleza yale yote aliyoyaasisi na akatumia fursa hiyo kutoa mkono wa pole kwa familia na Kanisa Anglican kwa ujumla.
Hayati Askofu Mkuu mstaafu John Ramadhan, mwenye umri wa miaka 90, alifariki dunia Septemba 12, 2022 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelezwa kwa ajili ya matibabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiagana na viongozi wa Kanisa la Anglikana Mkunazini Zanzibar, baada ya kumalizika kwa maziko ya Askofu mstaafu John Aukland Ramadhan yaliofanyika leo katika viwanja vya Kanisa la Mkunazini Wilaya ya Mjini Unguja jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news