Rais Samia atoa mkono wa pole kwa familia ya Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameifariji na kutoa mkono wa pole familia ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, kutokana na kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan kilichotolea juzi usiku katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja na kuzikwa jana Kijijini kwake Mangapwani Mkoa Kaskazini Unguja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Ali Hassan Mwinyi (kulia) alipofika kutoa pole kwa kufiliwa na mtoto wake marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi, Chukwani Nje ya Jiji la Zanzibar,Mkoa Mjini Magharibi (katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Rais) Mbunge wa Fuoni Mhe.Abass Ali Hassan Mwinyi.

Hafla hiyo ambayo iliambatana na dua ilifanyika nyumbani kwa marehemu Chukwani, Mkoa Mjini Magharibi, ambapo pia Mama Samia alipata fursa ya kutoa mkono wa pole kwa Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Mwinyi, Mama Siti Mwinyi , Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariam Mwinyi, Mke wa marehemu Fauzia Salim Hilali pamoja na wanafamilia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akimfariji na kumpa pole Bi.Fauzia Salim Hilal (katikati) kizuka wa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi mtoto wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi, nyumbani kwao Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar, kushoto ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Siti Mwinyi (kulia) Kizuka wa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Bi,Fauzia Salim Hilal (wa pili kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi (kushoto) wakiitikia dua iliyoombwa nyumbani kwa marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar.
Baadhi ya wanafamilia na watoto wa marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi mtoto wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Ali Hassan Mwinyi wakiitikia dua iliyoombwa nyumbani kwao Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar,wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mama Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) alipofika kutoa pole kwa msiba walioupata.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi na Mkewe Mama Siti Mwinyi (katikati) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) wakiitikia dua iliyoombwa na Sheikh Asumani Mohamed Jengo (kulia) nyumbani kwa Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B“ Nje ya Jiji la Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Rais Samia alimuomba Mwenyezi Mungu amsamehe marehemu madhambi yake na kumpumzisha kwa amani, huku akiwataka wafiwa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa mpendwa wao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news