SEHEMU YA 1: Tution ruksa mkoani Njombe, RC Mtaka afafanua

ANAANDIKA Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Athony Mtaka...,tumewaruhusu walimu wetu wawe huru kufundisha Tuition (masomo ya ziada) kwa kuanza na wanafunzi wanaomaliza darasa la saba mwaka huu.

Walimu waanzishe Pre-Form One kwa wazazi walio na utayari wa mtoto wake kujiandaa na masomo ya kidato cha kwanza ruksa kumpeleka mtoto wake,hii itasaidia watoto kutokaa bila kuwa na cha kufanya kwa miezi mitatu wakisubiri matokeo ya kidato cha kwanza.

Na pia washindani wetu wote hasa shule binafsi pamoja na kwamba wanachukua watoto waliofanya vizuri katika masomo yao bado watoto husika wanaokaa kwenye familia nyingi zilizo bora ama kifedha ama kiuelewa kiasi kwamba wanaenda form one wakiwa wengi wameshasoma nusu ya mtaala wa kidato cha kwanza.

Zipo shule baadhi za mashirika ya dini ambazo watoto wakishamaliza mitihani ya darasa la saba na wakafaulu mitihani ya shule hizo huanza Pre Form one kabla ya Form one rasmi,na ni takwa la lazima kwa shule husika na wazazi husika wanatimiza takwa hilo.

Hatujaona sababu ya kwa nini sisi Njombe tuzuie, pia tumejirdhisha pasi na shaka kwamba hakuna uhusiano kati ya utoro wa baadhi ya walimu kwenye vipindi vyao darasani na wao kufundisha tuition na kama kuna utoro wowote kwa walimu basi mashauri ya kinidhamu yashughulikiwe kama inavyokusudiwa,

Zaidi ya yote tumejiridhisha namna ambavyo kada zingine katika utumishi wa umma wanao uhuru wa kufanya kazi zao binafsi bila kuathiti mda wa mwajiri.

Mfano baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma wapo wanaofundisha vyuo vikuu zaidi ya kimoja, tunao watoa huduma kwenye sekta za afya za umma,wanatoa huduma zao kwenye hospitali zaidi ya moja,wanamiliki maduka yao ya madawa,wanamiliki hospitali zao.

Hivyo hivyo katika kada za sheria,uhasibu,uhandisi kwenye ofisi za umma wanafanya kazi zao katika muda wao binafsi, bado sijaona dhambi Mwalimu wa Njombe akiwa kwenye likizo ndefu ya Juni-Julai,Desemba-Januari asifundishe Tuition kwa wanafunzi wa Pre Form one,wanafunzi wanaorudia mitihani yao.

Pia wanafunzi wa QT,wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya taifa,kidato cha nne au cha sita, tuition hazifundishwi maeneo binafsi,au muda wa masomo,na pia vijana waliosoma shahada za ualimu na hawajapata ajira...


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news