SEHEMU YA 2 NA MWISHO: Tution ruksa mkoani Njombe, RC Mtaka asema itafanyika kitaaluma

ANAANDIKA Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Athony Mtaka...,Bonyeza hapa kusoma chapisho lililopita;
Vijana waliosoma shahada za ualimu na hawajapata ajira,nawahamasisha kuungana na walimu wanaotaka kufundisha Tuition ili watambulike na kuepusha wanafunzi kufundishwa na watu makanjanja, tumerasimisha jambo hili ili kuepukana na tuition za magendo, kuwaepusha watoto kuwa wazururaji, nyakati za likizo na wengine kujiiingiza kwenye makundi yasiyofaa.

Maeneo ya kufundishia Tuition itakuwa maeneo ya shule baada ya vikao vya bodi ya shule husika kukubaliana namna nzuri ambayo wahusika watachangia kwa kutumia madarasa na viti vya shule ili kama kuna uharibifu basi mchango husika utatumika.

Ni jambo la faraja tutakapoona vijijini kuna mabango yanayohamasisha elimu,uwepo wa Pre form one au ufundishwaji kwenye masomo ya sayansi kwa kutumia maabara zinazotembea,kuliko kuwa na vijiji ambavyo kuna mabango yanayohamasisha nguvu za kiume au usafishaji nyota au dawa za kurudisha ndoa zilizopotea,utajiri au upandaji vyeo kupitia waganga wa kienyeji...

KUHUSU WATOTO wa kidato cha nne,tumewaelekeza wakuu wa shule wapitie matokeo ya wanafunzi waliopo kidato cha nne,na kama kuna waliopata daraja sifuri (Division Zero) wakiwa form three kuingia form four,na wakiwa form four mitihani yote ya majaribio (Pre Mock,Mock) walipata Division Zero,basi wapunguziwe masomo yao ili wabaki na masomo matano ya kujiandaa na mitihani ya taifa.

Busara imetuongoza kwa mfano,mwanafunzi amepata Alama F toka anaanza form one mpaka form four katika masomo ya Physics, Mathematics, Chemistry, Biology, basi wanafunzi hawa waandaliwe katika masomo matano ya History, Civics, Kiswahili, Kiingereza, Geography.

Ili waweze kutilia mkazo walau wabahatishe alama za kuweza kuwasaidia kupata cheti badala ya kutoka na sifuri na hasa katika ulimwengu tulionao ambapo ajira nyingi leo cheti cha kidato cha nne kinapewa nafasi zaidi kuliko hata ujuzi wa muhusika.

Kiujumla tunajiandaa kama mkoa kuwa na kamati imara na bora za kitaaluma ambazo wanafunzi wetu watakuwa wakiandaliwa vizuri,mkoa ambao walimu wetu watapewa daraja la juu katika kuheshimiwa na kuthaminiwa.

Matarajio ni kuona mbele ya safari mkoa wetu unaongoza mitihani yote ya Taifa, darasa la nne,darasa la saba,kidato cha pili,kidato cha nne,kidato cha sita,shule 10 bora na baadae wanafunzi 10 bora.Wakati wa Mungu Utasema-Tupeni nafasi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news