TPA mbioni kuanza ujenzi Bandari ya Bagamoyo

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema ipo katika maandalizi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, itakayosaidia utoaji wa huduma za upakiaji na kushusha mzigo.
Wakati huo huo, TPA mesema kuanzia Januari mwaka 2023 itaanza ujenzi wa kituo kikubwa cha kisasa cha kupokelea mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, hatua itakayosaidia meli kutotumia muda mrefu kushusha.

Plasduce Mbossa ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA amesema hayo jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na ujumbe wa Bodi ya Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), waliofika kutaka kujua mipango mbalimbali ya mamlaka hiyo katika kuboresha utoaji wa huduma.

Mwenyekiti wa Bodi ya EABC, Anjelina Ngalula, alisema yeye pamoja na wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wako tayari kutumia Bandari ya Dar es Salaam katika kushusha mizigo yao, kwa kuwa malalamiko yaliyokuwepo awali yamefanyiwa kazi.

Aidha, Mbossa amesema, ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ulikuwa umefikia hatua ya kuzungumza na mwekezaji, lakini ghafla alijitoa na kwa sasa wameanza mchakato wa kutafuta mwingine.

Pia amesema mbali ya kutafuta mwekezaji, lakini sehemu ya mradi wa ujenzi wa bandari hiyo utafanywa na mamlaka hiyo wenyewe, lengo kubwa ni kupunguza muda wa meli kusubiri kushusha mizigo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news