Waziri Mkenda:Ratiba ya kufunguliwa shule ipo pale pale, hakuna maelekezo mengine

NA MATHIAS CANAL-WEST

SERIKALI imekanusha taarifa za uzushi zilizotolewa kuhusu tarehe ya shule kufunguliwa iliyotolewa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na sekta ya elimu nchini.
Taarifa hiyo imeenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikieleza kuwa shule zitafunguliwa tarehe 21 Septemba 2022 jambo ambalo sio sahihi na hakuna muongozo wala maelekezo hayo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekanusha uvumi huo leo Septemba 3, 2022 wakati akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Skuli ya Ole Sekondari iliyopo katika Mkoa wa Kusini Pemba jijini Zanzibar wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja visiwani humo.
Waziri Mkenda ameeleza kuwa ratiba ya kufunguliwa shule ipo vilevile kwa mujibu wa Waraka wa Elimu Na 2 wa mwaka 2022 kuhusu mihula ya masomo uliotolewa na Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Lyabwene Mtahabwa.

“Naomba mpuuze jambo hili kwanza aliyesambaza anatumia nembo ya kampuni moja ambayo kampuni hiyo haijui na haihusiki na tangazo hilo, kwa hiyo hakuna maelekezo yoyote zaidi ya yale yaliyotolewa na Kamishna wa Elimu,"amemesema Waziri Mkenda.Kuhusu mageuzi ya elimu, Waziri Mkenda amesema kuwa serikali inafanya mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 pamoja na mapitio ya mitaala ili kuboresha sekta ya elimu.
Amesema kuwa, Tanzania Visiwani (Zanzibar) na Tanzania Bara zinafanya kwa pamoja mapitio hayo kwa karibu ili kupata mawazo ya wadau wa elimu na wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyeitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha inaboresha elimu hususani kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wanakuwa na elimu ufundi na elimu ujuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news