Waziri Mkuu amwakilisha Rais Samia kwenye maziko ya Shinzo Abe nchini Japan

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maziko ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe. Pichani Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mkoani Dar es Salaam.

Taratibu za kutoa heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika Jumanne, Septemba 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Nippon Budokan. Waziri Mkuu huyo mstaafu aliuawa Julai 8, mwaka huu kwa kupigwa risasi akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika jiji la Nara nchini humo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maziko ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe. Pichani Waziri Mkuu, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mkoani Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Bw. Abe ambaye anatajwa kuwa kiongozi aliyeshika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kwa muda mrefu katika historia ya Japan, aliingia madarakani kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 na akarudi tena mwaka 2012 hadi 2020.

Akiwa Japan, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Fumio Kishida.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news