ALHAJ OTHMAN, VIONGOZI NA WANANCHI WA ZANZIBAR WAADHIMISHA MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

NA DIRAMAKINI
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman usiku wa Oktoba 8, 2022 amejumuika katika hafla ya Maulid ya Kitaifa, Viwanja vya Maisara Suleiman, Mkoa wa Mjini-Magharibi Unguja, akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kuadhimisha Mazazi ya Kiongozi wa Umma wa Kiislamu, Mtume Muhammad (SAW).
Alhaj Othman ambaye ni Mgeni Rasmi wa Hafla hiyo, amejumuika na Viongozi wa Kitaifa wa Serikali, Dini, Mashirika ya Kitaifa, Wanadiplomasia, Vyama vya Siasa, Jamii, na Maelfu ya Wananchi kutoka Maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.
Wengine waliohudhuria hapo ni pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Alhaj Hemed Suleiman Abdulla; Rais Mstaafu wa Awamu ya Saba ya Zanzibar, Alhaj Dokta Ali Mohamed Shein; Makamu wa Pili Mstaafu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Ramadhan Abdalla; Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mahmoud Mussa Wadi; Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali; na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana, Sheikh Abdalla Talib Abdalla.
Katika hafla hiyo amehudhuria pia Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Zainab Kombo Shaib; Mawaziri mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Bi Mgeni Hassan Juma.

Post a Comment

0 Comments