Balile asisitiza weledi na nidhamu kwa wanahabari

NA DIRAMAKINI

WANAHABARI nchini wametakiwa kuzingatia weledi na nidhamu ya hali ya juu ili kuifanya taaluma ya habari nchini ambayo ni mhimili wa nne wa dola usiyo rasmi uendelee kuheshimika.

Rai hiyo imetolewa leo Oktoba 20, 2022 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatius Balile katika mafunzo maalum kwa wahariri na wanahabari yanayoangazia uchechemuzi wa sheria za vyombo vya habari nchini.

Wadau wa vyombo vya habari nchini wanaamini wakati Serikali ikiwa katika mchakato wa kufanyia maboresho sheria na kanuni kandamizi zinazozuia vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa uhuru ili waandishi waweze kutimiza wajibu wao, pia ni jukumu la wanahabari kuzingatia weledi na nidhamu.

"Hivyo, tukifanya hayo taaluma hii tutairejesha katika hadhi ambayo kila mwanahabari atafanya kazi kwa kuheshimiwa na kupewa hadhi kubwa na jamii katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku,"amesisitiza.
 
Pia amesema, licha ya shauku ya wengi kutaka kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zipo baadhi ya sheria ambazo zinasababisha washindwe kufanya kazi zao kwa weledi na hivyo kushidwa kutetea haki na maslahi yao nchini.

Amesema, waandishi wa habari wenyewe ndio wamavaa viatu na wanafahamu mazuri na mabaya wanayokutana nayo kwenye tasnia, hivyo wakiandika na kuyasemea matatizo wanayokutana nayo itaifanya Dunia itambue changamoto za waandishi wa habari.

"Kuna baadhi ya taasisi zinasema wanatetea haki za waandishi, lakini wao sio waandishi na hawazijui changamoto za waandishi ndio maana tukasema tuanze kutetea haki na maslahi yetu wenyewe kwa ustawi bora wa tasnia hii.

"Ili kutetea haki zetu zipatikane tukiwa na hali nzuri basi tutakua na nguvu ya kutetea haki za wengine kwa ufasaha pia tuondoe ile kasumba ya kwamba wanahabari hatuandiki habari zinazotuhusu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news