Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi leo Oktoba 20, 2022.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said imeeleza kuwa, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Is-haka Ali Khamis kuwa Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Zanzibar.

Kabla ya uteuzi huo ambao unaanza leo, Mheshimiwa Is-Haka alikuwa Naibu Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi Unguja.

Post a Comment

0 Comments