IJP Wambura afanya mabadiliko makamanda, uhamisho

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camillus Wambura amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi mikoa na mmoja kumhamishia makao makuu ya Polisi Dodoma.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 20, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SACP David Misime.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, IJP Wambura amewahamisha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Henry Mwaibambe ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.

Aidha, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Safia Shomary amehamishiwa Mkoa wa Geita kuwa Kamanda wa Polisi mkoani humo.

Pia aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Richard Ngole amehamishiwa makao makuu ya Polisi Dodoma.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi yake imechuuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Kungu Malulu ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news