Rais Samia afanya uteuzi NIMR

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 20, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus imefafanua kuwa, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Prof.Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMRI na uteuzi wake umeanza Oktoba 19, 2022.

Prof.Aboud ni Profesa Mshiriki, Mhadhiri Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam.

Aidha, Prof.Aboud kwa mujibu wa taarifa hiyo anachukua nafasi ya Prof.Yunus Daud Mgaya ambaye amemaliza muda wake Septemba, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments