Leo ni kumbukizi ya Mfalme wa Kwanza Mwanamke duniani kuiongoza Poland


Picha na halfarsedhistory.

JADWIGA anayejulikana pia kama Hedwig, alikuwa mfalme wa kwanza wa kike wa Ufalme wa Poland, alitawala kutoka Oktoba 16, 1384 hadi kifo chake Julai 17, 1399.

Jadwiga alikuwa binti wa Louis I, mfalme wa Hungary na Poland, na Elizabeth wa Bosnia. Baada ya kifo cha Louis mnamo Septemba 11, 1382, binti yake mkubwa, Maria, alichaguliwa kuwa malkia wa Hungary, lakini Wapolandi waliamua kumaliza umoja wa kibinafsi kati ya nchi hizo mbili kwa kumchagua Jadwiga kama malkia wao, ingawa wakati huo alikuwa mtoto wa miaka 10. Oktoba 16, 1384, alitawazwa kuwa Mfalme wa Poland.

Alikuwa Mfalme wa Poland badala ya malkia kwa sababu, kwa sheria mtawala alipaswa kuwa Mfalme. Mjomba wake mkubwa, Mfalme Casimir III hakuwa na watoto wake wa kiume.

Post a Comment

0 Comments