Naibu Spika Zungu ashiriki maziko ya Mbunge wa Jimbo la Amani

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu ameshiriki katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Amani (CCM) Mhe. Mussa Hassan Mussa yaliyofanyika jioni ya Oktoba 13, 2022 Kijijini kwao Bwejuu, Zanzibar.

Mheshimiwa Mussa Hassan Mussa ambaye alizaliwa Februari 11, 1959 amefariki Oktoba 13, 2022 ambapo alihudumu katika nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kwa nyakati tofauti.

Post a Comment

0 Comments