NAIBU WAZIRI MASANJA AWATAKA WANANCHI NJOMBE KUWA WAHIFADHI

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (MB) amewataka wakazi mkoani Njombe kuwa Wahifadhi kwa kuacha tabia ya kukata miti ovyo na kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi

Ameyasema hayo Oktoba 27,2022 katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye Kijiji cha Mpanga, Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe.
“Niwaombe tulilinde Pori la Akiba la Mpanga Kipengere, tuwe wahifadhi wazuri, tusiende kukata miti hovyo, tusiingie ndani na kuvamia vyanzo vya maji kwa sababu vinasaidia upatikanaji wa maji safi na salama,” amesema.

Naibu Waziri Masanja amewatahadharisha wananchi kutoyasogelea maeneo ya Hifadhi kwa kuwa yana wanyamapori ambao ni hatari kwa binadamu.
Pia, amewaasa kuacha mtindo mbaya wa kusafisha mashamba kwa kuchoma moto,ili kuepuka moto kusambaa katika mashamba ya miti.

Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta imemalizika mkoani Njombe ambapo itaendelea na shughuli za utatuzi wa migogoro ya ardhi Oktoba 28,2022 mkoani Ruvuma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news